Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Group, Abdulmajid Nsekela amesema upanuzi wa CRDB Bank marathon katika nchi za DRC na Burundi unenda sambamba na malengo ya benki ya kujitanua kikanda na kuchochea maendeleo barani Afrika.
Nsekela amesema, Benki ya CRDB imejipanga kikamilifu kusaidia kuweka mazingira wezeshi na kuwawezesha Wananchi katika nchi inapotoa huduma kunufaika na fursa malengo ya Afrika Tuitakayo “The Africa We Want” 2063.
Nsekela amesema mafanikio ambayo Benki ya CRDB imeyapata katika nchi za DRC na Burundi yanatokana na mahusiano mazuri baina ya Tanzania na nchi hizo yakichagizwa na uongozi mahiri wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Burundi Evarist Ndayishimye, na Rais wa DRC Congo chini ya Mhe. Rais Félix Tshisekedi.