Siku chache baada ya kutajwa na mtandao wa habari za michezo wa Goal.com kuwa mwanasoka tajiri kuliko wote Ulimwenguni, Cristiano Ronaldo amefanya kitendo ambacho kimezidi kumpatia sifa ya kuisadia wale wenye matatizo.
Kwa mujibu wa gazeti la kihispania AS ni kwamba Ronaldo ameamua kumlipia fedha za matibabu mtoto mwenye miezi 10 Erik Ortiz Cruz ambaye ni mgonjwa sana akisumbulia na matatizo kwenye ubongo wake (Cortical dysplasia.)
Kutokana na taarifa za kitabibu ugonjwa huu kawaida humfanya mtu awe anapata mshtuko unaoweza kupelekea kuzimia mara 30 kwa siku, hivyo kutokana na hali hiyo mtoto unamfanya mtoto huyo anahitaji kufanyiwa upasuaji ili kuondoa hali hiyo isiyo ya kawaida kwenye ubongo.
Kila kipimo anachofanyiwa mtoto huyo kina gharama ya 6,000 euros na upasuaji mzima unagharimu kiasi cha 60,000 euros hivyo watu wa kijiji cha Villaluenga de la Sagra, Spain, wamekuwa wakijaribu kukusanya fedha kwa ajili ya matibabu ya mtoto huyo kupitia michango.
Jambo hili lilipomfikia Ronaldo ambaye alifuata aweze kutoa jezi yake na viatu vyake ili vipigwe mnada, akawapa walichotaka kwa ajili ya mnada na kisha akalipia gharama zote za matibabu ya mtoto huyo.