Crystal Palace na Newcastle wapo kwenye mazungumzo kuhusu kumnunua Marc Guehi.
Beki huyo yuko kwenye rada za Newcastle baada ya kufanya vyema kwenye michuano ya Euro 2024 akiwa na England msimu huu wa joto.
Guehi amebakiza miaka miwili tu kwenye mkataba wake na kuna imani Palace inaweza kujaribiwa kuuza.
Newcastle sasa wameanzisha mazungumzo na The Eagles na wanatumai kuwa dili linaweza kukamilika haraka kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu wiki ijayo.