Meneja Masoko Mwandamizi wa Kampuni ya Coca-Cola Tanzania, Kabula Nshimo (kushoto), akisalimiana na Mratibu wa Tamasha maarufu la vyakula ‘International Food Carnival’, Moureen Ian, wakati wa uzinduzi wa tamasha hilo leo jijini Dar es Salaam.
Tamasha hili linalotarajiwa kufanyika kwa siku mbili mfululizo, tarehe 19 na 20 ya mwezi huu, katika viwanja vya Farasi, Oysterbay, Dar es Salaam. Coca-Cola Tanzania ni miongoni mwa wadhamini wakuu wa tamasha hili ambalo linalenga kuwaleta pamoja wapenda vyakula na burudani kutoka maeneo mbalimbali.