Mamlaka ya Cuba ilisema kuwa imewakamata watu 17 kwa tuhuma zinazohusiana na kundi la wasafirishaji haramu wa binadamu ambao wanadaiwa kuwashawishi vijana wa Cuba kuhudumu katika jeshi la Urusi huku kukiwa na mzozo wa Ukraine.
Cuba mapema wiki hii ilifichua mamlaka zilikuwa zikifanya kazi “kutenganisha na kusambaratisha” mtandao huo, ambao ilisema ulifanya kazi katika ardhi ya Cuba na Urusi.
“Kutokana na uchunguzi huo, watu 17 wamekamatwa hadi sasa, miongoni mwao wakiwa ni mratibu wa ndani wa shughuli hizi,” Cesar Rodriguez, kanali wa wizara ya mambo ya ndani ya Cuba, alisema siku ya Alhamisi katika kipindi cha televisheni.
Wale wanaohusika wanaweza kuadhibiwa hadi miaka 30 jela, kifungo cha maisha au adhabu ya kifo, kutegemeana na ukali na aina ya uhalifu, ambayo ni pamoja na biashara haramu ya binadamu, mapigano kama hatua ya mamluki na uadui dhidi ya taifa la kigeni.
Cuba inasema haina sehemu katika vita vya Ukraine, na kwamba inakataa matumizi ya raia wake kama mamluki.