September 23 2016 Msajili wa vyama vya siasa alitoa msimamo na ushauri wake baada ya kupokea malalamiko na kupitia maelezo ya pande zote kuhusu mgogoro wa uongozi uliopo kwenye chama cha wananchi CUF.
Baada ya upembuzi Msajili wa Vyama vya saisa Jaji Mutungi alitoa mwongozo kuwa Prof. Lipumba bado ni mwenyekiti halali wa chama hicho aidha baadhi ya viongozi na wanachama waliokuwa wamesimamishwa na wengine kufukuzwa, Jaji mutungi amesema ni wanachama halali.
Chama cha wanachi CUF kimekiri kupokea kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa msimamo na ushauri wa vyama vya siasa kuhusu mgogoro wa uongozi wa kitaifa wa Chama cha CUF ambao uliwasilishwa Ofisi Kuu ya Chama, Buguruni, jana usiku.
Baada ya kupokea Ushauri huo CUF kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari wameyaeleza haya……..
>>>Sheria ya Vyama vya Siasa (Political Parties Act, No. 5 of 1992) haimpi mamlaka wala uwezo wowote Msajili wa Vyama vya Siasa kutoa ushauri, msimamo au mwongozo kwa vyama vya siasa kuhusiana na maamuzi ya vikao vya Chama.
>>>Kwa msingi huo huo, tunawataka wanachama wa CUF na wananchi wote kutambua kwamba Msajili hana uwezo kisheria wa kusikiliza mashauri yanayohusiana na malalamiko dhidi ya maamuzi ya vikao vya vyama vya siasa na kuyatolea uamuzi. Uwezo huo ni wa Mahakama. Hivyo tunawataka wanachama wa CUF na wananchi wote kupuuza ushauri huo wa Msajili.
>>>Chama kinasisitiza tena kwamba maamuzi ya Mkutano Mkuu Maalum wa Taifa wa tarehe 21 Agosti, 2016 na Baraza Kuu la uongozi la Taifa la tarehe 28 Agosti, 2016 ni halali na yako pale pale na kwamba Prof. Ibrahim Lipumba si Mwenyekiti wa CUF na wanachama waliosimamishwa au kufukuzwa wataendelea kubakia wamesimamishwa au kufukuzwa isipokuwa tu iwapo vikao vya Chama vitakapofanya maamuzi mengine.
ULIKOSA HAYA MAPOKEZI YA PROF. LIPUMBA OFISI YA MAKAO MAKUU YA CUF? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI