Baada ya headline za Chama cha wananchi CUF kuwavua uanachama baadhi ya wanachama wake akiwemo aliyewahi kuwa mwenyekiti wake Profesa Ibrahim Lipumba leo September 15 2016 kamati ya uongozi taifa imekutana na waandishi wa habari Dodoma na kuzungumzia hatma ya chama hicho ikiwa ni pamoja na kumtaka msajili wa vyama vya siasa asitumike kukiyumbisha chama hicho.
Chama cha CUF kimemtaka msajili wa vyama vya siasa nchini asitumike kukiyumbisha chama hicho kwa madai baadhi ya vyama vinatumia ofisi yake
— millardayo (@millardayo) September 15, 2016
'Baraza kuu CUF liliwavua uanachama wanachama kadhaa akiwemo Prof Lipumba na kuwaandikia barua, tunaunga mkono hatua hiyo ya kinidhamu' #CUF
— millardayo (@millardayo) September 15, 2016
'Tuna taarifa za Prof Lipumba kupeleka malalamiko yake kwa msajili wa vyama vya siasa akijitangaza kuwa yeye ni M/kiti halali wa CUF' #CUF
— millardayo (@millardayo) September 15, 2016
'Ifahamike kuwa sisi CUF hatumtambui Prof Lipumba kuwa M/kiti wetu na kwasasa chama kinaongozwa na chama taifa chini ya Julius Mtatiro' #CUF
— millardayo (@millardayo) September 15, 2016
ULIMIS MSIMAMO WA PROFESA LIPUMBA KUHUSU KUFUKUZWA KWAKE CUF