Hivi ni moja ya vitu ambavyo ninapokutana navyo, moja kwa moja nafikiria kukufikishia na wewe pia, hivi unajua kikombe kinaweza kupima aina ya kinyaji unachokunywa?
Haya ndiyo maendeleo ya kiteknolojia ambapo unaambiwa hiki kikombe kina uwezo wa kupima cafeine kutoka iliyopo kwenye kinywaji unachokunywa, pamoja na kitu kingine chochote ambacho kimo ndani ya kinywaji hicho hata kama ni kilevi, iwapo ukanywa halafu ukashusha kikombe chini na una kiu bado kinakupa ishara kwamba unatakiwa unywe tena kinyaji unachokunywa.
Kikombe hicho kinatumia app maalum ambapo unaweza kukifanyia sync kupitia Bluetooth, iPhone Operating System na Android app, unaweza kukichaji kwa Wireless, kina uwezo wa kukaa na chaji kwa muda wa siku tano mpaka siku saba na kinaweza kuingia chupa moja ya soda ya kawaida.
Tazama video hii kujua mengine ambayo kikombe hiki kinayafanya.
https://www.youtube.com/watch?v=lu4ukHmXKFU
Watengezaji wa kikombe hiki wanakiita Vessly, kitaanza kuuzwa mwakani na kitapatikana kwa kiasi cha dola 99 tu.
Hakika utapata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook