Kutoka nchini Sudan Kusini, ripoti ya Umoja wa Mataifa leo February 23, 2018 inaeleza kuwa watoto nchini humo wanalazimishwa kutazama jinsi mama zao wanavyotendewa vitendo vya ubakaji na wengine wakiuawa.
Ripoti ya wachunguzi wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa maafisa 40 wanaweza kuhusishwa katika uhalifu wa vita na uhalifu wa aina nyingine unaoendelea nchini humo dhidi ya binadamu.
Inaelezwa kuwa raia wamekuwa wakiteswa na kuharibiwa na vijiji vikiharibiwa. Migogoro kati ya vikundi vya serikali imeendelea Sudan Kusini pamoja na mpango wa amani uliosainiwa mwaka 2015.
Hali ilivyo Rombo katika Msiba wa Akwilina, Prof.Ndalichako kuyaongoza Mazishi
Ufafanuzi wa Kamanda Msangi, watu kupingwa nondo Mwanza.