Mitandao ya kijamii inazungumziwa kwa namna mbalimbali, wengine wakisema haina manufaa na inasabisha matatizo kwenye jamii, wapo wanaosema kuwa ni ya muhimu na ina manufaa hususani kwa jinsi teknolojia inavyoendelea kukua.
Mwanamke mmoja ameeleza jinsi gani mtandao wa FaceTime ambao ni wa kupiga simu ya video, umeokoa maisha yake.
Mwanamke huyo Adumea Sapong, 58, mkazi wa Manchester Uingereza alikuwa amepigiwa simu hiyo na mdogo wake Opokua Kwapong anayeishi Mji wa New York Marekani na katikati ya maongezi yao akapata kiharusi (stroke).
Akisimulia kisa hicho Opokua anasema alimpigia simu dada yake huyo na wakiwa wanaongea aligundua kuwa uongeaji wake ulikua wa kuzorota sana, na hata alivyomwambia akasema ni kawaida tu.
Opokua anasema wakiwa wanaendelea kuongea alianza kuona sura ya dada yake ikibadilika na ndipo alipohisi kuna kitu hakiko sawa na kuwambia apige simu ya tahadhari 911 ili apewe msaada.
Baada ya Sapong kupiga simu hiyo na kufuatwa nyumbani kwake anapokaa peke yake na kupelekwa hospitali, alipimwa na kugundulika kuwa kulikuwa na ‘kuvilia damu’ kwenye ubongo, na kiharusi hicho kikamsababishia kupooza upande wa kushoto wa mwili wake.
Baba Mzazi wa Akwilina aomba kuonana na JPM, amesema ana siku 4 hajaoga
Ombi la Mbunge Rombo Selasini akiwa na Wazazi wa Akwilina, kwa Serikali