China na Sheria zao, Serikali ya nchi hii ni moja kati ya chache ambazo zimekuwa mstari wa mbele kwenye utekelezaji wa chochote kile ambacho watakiamua, kwa wakati wowote na kwa njia yoyote.
Moja ya stori za mwisho mwisho kusikika kutoka China ni ishu ya kila mtu kutakiwa kujisajili kwenye mitandao ya kijamii kwa majina yote halali yani, yale ambayo yanatambulika kwenye cheti cha kuzaliwa au passport hivi.
Kuna hii nyingine ya kuhusu hiyo hiyo mitandao, unaambiwa Mamlaka ya Mawasiliano China wamefuta website 65 ambazo watu walizitumia kwa masuala ya mapenzi ikiwemo kutafuta wapenzi na kushare picha za ngono.
Mitandao hiyo iligundulika kwamba watu walikuwa wakijisajili kwa majina fake, halafu wanashare picha, video za ngono pia.
Rungu limeanza kazi ndani ya China, yeyote anayetaka kuendelea kutumia mitandao ya kijamii lazima ajisajili kwa jina lake kamili, hii itakuwaje mfano ikianza Bongo kwa kasi hii hii mtu wangu!
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook