Mbunge wa Kigoma Kusini Hasna Mwilima alipata nafasi kusimama Bungeni Dodoma leo April 12, 2018 kwa ajili ya kuchangia mapendekezo katika ya Wizara ya TAMISEMI ambapo kati ya vitu alivyoiomba Serikali kuyafanyia kazi ni changamoto ya huduma za kiafya katika jimbo lake.
Hasna Mwilima amesema…>>>“Nina vituo viwili vya afya katika jimbo langu ambapo tuna upungufu wa wauguzi ikiwemo madaktari, wananchi wangu wanatembea kwa zaidi ya km 250 kwa ajili ya kutafuta huduma ya afya pekee, kiukweli hali ni mbaya mbaya sana”
Umekerwa na ubovu wa Barabra ya Pamba Mwanza, Good News hii hapa