Mtanzania Mbwana Samatta anayeichezea club ya KRC Genk ya Ubelgiji leo atakuwa anacheza kwa mara ya pili michuano ya Europa League akiwa na club yake ya KRC Genk itakayocheza dhidi ya Malmo ya Sweden club ambayo ni chimbuko la mshambuliaji wa zamani wa Man United Zlatan Ibrahimovic.
Samatta leo watacheza na Malmo wakiwa nyumbani kwao Luminus Arena, kuelekea game hiyo Ayo TV imempata Mbwana Samatta katika exclusive interview, unajua Samatta hadi sasa ameichezea Genk game zaidi ya game 40.
Katika zaidi ya game 40 za mashindano yote aliyowahi kuichezea Genk katika michuano mbalimbali, ameitaja game ya Europa League kati ya Genk dhidi ya Sassuolo ya Italia wakiwa katika uwanja wa nyumbani, ndio game yake ngumu zaidi ambayo amewahi kucheza akiwa na Genk.
EXCLUSIVE: Licha ya kuwa na pesa na ustaa, hii ndio Sababu inayomfanya Samatta asiringe