Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imesema iko mbioni kuanza kufanya marekebisho ya bandari ya Dar es salaam ikiwemo kuongeza kina cha bahari kwenye eneo la kupakia na kushushia mizigo bandarini.
Taarifa hii imetolewa na Waziri Prof. Makame Mbarawa leo November 17, 2016 wakati wa mkutano na wadau kutoka sekta zinazohusiana na Wizara ili kuona utendaji wa wizara hiyo kwa mwaka mzima na jinsi ya kutatua changamoto mbalimbali.
Profesa Makame Mbarawa amesama kuwa Serikali inakamilisha utaratibu wa kukopa fedha kutoka Benki ya Dunia ili kuanza ukarabati wa gati 7 za bandari hiyo. Pia Waziri amezungumzia Wizara hiyo kuanza kuboresha utaratibu wa jinsi ya kukuta tiketi za ndege za ATCL.
“Hatuwezi kuendelea kusema sababu ni World Bank wakati mradi haundi, inatakiwa tufike pahala tuone mradi unaenda na watu wanaona matunda ya mradi ule. Bandari ya Dar es salaam ni sehemu muhimu sana kwa uchimi wa Tanzania kama unavyojua inachangia asilimia 5 ya pato la taifa” – Waziri Makame Mbarawa
Taarifa kamili iko kwenye Video hii. Bonyeza Play kutazama.
VIDEO: Ipo hapa Ndege ya kipekee iliyonunuliwa na Serikali ya Rwanda, naambiwa iko moja tu Afrika nzima. Tazama hapa