Mbunge wa Handeni Vijijini Mboni Mhita ni miongoni mwa Wabunge waliopata nafasi ya kusimama bungeni Dodoma kuchangia mapendekezo yake katika bajeti ya Wizara ya TAMISEMI ambapo alilieleza Bunge namna halmashauri yake iinavyoshindwa kukamilisha baadhi ya miradi kwa sababu ya rushwa.
“Ni ukweli usiofichika kwamba Rushwa inachangia umasikini kwa hali ya juu sana, nayasema haya kwasababu nimeona namna wakinamama katika Jimbo la Handeni vijijini wanavyohangaika na tatizo la maji ambalo kulikuwepo na miradi mingi ya kuwezesha maji ambao hadi leo hakijafanyika kitu kwasababu ya rushwa zilizotawala ikiwemo ufujaji”
“Bila Kikwete, Mimi nisingekuwa Rais nakushukuru, SITOKUANGUSHA”- Rais Magufuli