August 02 2016 Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es salaam imetangaza tarehe 28 August 2016 kuwa ndio siku itakayoanza kusikiliza kesi inayomkabili mbunge wa Singida mashariki Tundu Lissu baada ya kupata maelezo ya tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi dhidi ya Rais John Pombe Magufuli.
Akisomewa maelezo ya awali na Hakimu wa mahakama hiyo Yohana Yongolo Inadaiwa June 28 2016 Tundu Lissu alitoa maneno ya uchochezi nje ya mahakama ya Kisutu.
Baada ya kusomewa maelezo Tundu Lissu, nje ya mahakama kaongea na waandishi wa habari.
ULIIKOSA ALICHOZUNGUMZA TUNDU LISSU BAADA YA KUPATA DHAMANA