Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam tarehe 17 Julai, 2024 lilitoa taarifa kuhusu dada wa kazi kufanya tukio baya la kikatili la kumjeruhi kwa kitu chenye ncha kali maeneo ya shingoni mtoto Malick Hashim anayeishi eneo la Goba Kinzudi, Kinondoni.
Baada ya tukio mtuhumiwa alikimbia.
Upelelezi wa tukio hilo la kikatili ulianza mara moja na tarehe 21 Julai 2024 saa 4:00 usiku Jeshi la Polisi lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo aliyekuwa mfanyakazi wa nyumba wa ndani aitwaye Cleminsia Cosmas Mirembe mwenye miaka 19 akiwa amejificha kwenye “pagala” maeneo ya Goba Kizudi Kinondoni.
Akiongea na waandishi wa Habari Kamanda wa polisi kanda Maalum ya Dar es salaam SACP Jumanne Murilo amesema mtuhumiwa huyo anahojiwa kwa kina na atafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo kwa hatua zaidi za kisheria.
Aidha Kamanda Murilo ametoa wito na kuwawashauri wazazi, walezi, walimu, na jamii kwa ujumla kuwafundisha watoto kujenga tabia ya kutembea katika makundi lakini pia watoto wasikubali kuwakaribu na watu wasiowafahamu, watoto wasitumwe maeneo ambayo kwa mazingira ni hatarishi ikiwa ni pamoja na kuacha kuwatuma watoto wadogo maeneo mbalimbali nyakati za usiku