Gao Yaojie, daktari mashuhuri mpinzani ambaye alifichua janga la Ukimwi vijijini nchini China, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 95.
Dk.Gao alifariki huko New York, ambapo alikuwa uhamishoni tangu mwaka 2009, rafiki yake aliiambia BBC.
Kazi yake ilifichua jinsi biashara za kuuza damu zilivyosababisha kuenea kwa VVU mashambani.
Alikuwa mstari wa mbele katika harakati za Ukimwi nchini China na alisafiri kote nchini kutibu wagonjwa, mara nyingi kwa gharama zake mwenyewe.
Alizaliwa katika jimbo la Shandong mwaka wa 1927, yeye na familia yake walikimbilia jimbo la kati la Henan wakati wa Vita vya Pili vya Dunia.
Daktari wa magonjwa ya wanawake kwa mafunzo, alikutana na mgonjwa wake wa kwanza wa Ukimwi katika jimbo la kati la Henan mnamo 1996.
Katika miaka ya 1980 na 1990, uuzaji wa damu ulikuwa wa kawaida katika maeneo ya vijijini kama vile Henan.
Fursa chache za kiuchumi miongoni mwa jumuiya za wakulima ziliwaacha na chaguzi nyingine chache za kujikimu kimaisha na uuzaji wa damu mara nyingi uliungwa mkono na serikali za mitaa.
Lakini kutokana na visa vichache vya VVU kugunduliwa vijijini China wakati huo, na uelewa mdogo wa Ukimwi, damu pia ilikusanywa kutoka kwa wagonjwa wa VVU, na kusababisha kuenea kwa ugonjwa huo.
Wakati huo, mamlaka za China zilifikiri kwamba VVU iliambukizwa kwa njia mojawapo kati ya mbili , kupitia ngono au kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa ujauzito.
Ameandika vitabu kadhaa kuhusu UKIMWI pamoja na mkusanyiko wa mashairi.
Katika mahojiano kabla ya Siku ya Ukimwi Duniani siku ya Alhamisi, Dk. Gao alizungumza kuhusu maisha yake nchini Marekani na kile anachokiona kuwa ukweli ambao bado haujajulikana kuhusu janga la UKIMWI nchini China.