Daktari wa meno huko Wisconsin Marekani amepatikana na hatia ya makosa matano ya ulaghai wa huduma ya afya baada ya kugundulika kuharibu meno ya Wagonjwa kwa makusudi ili kujipatia pesa nyigi zaidi.
Dr. Scott Charmoli (61) amekua akiwaonesha Wagonjwa wake picha za X-ray za meno yao na kuwafanya waamini ni mabovu na yamevunjika au kuoza “Wagonjwa ambao waliamini Charmoli ndiye Mtaalam walikubali uwasilishaji wake wa uwongo na kukubaliana na utaratibu wa kulipia” imeeleza nyaraka ya Mahakama.
Charmoli amekua akivunja jino la Mgonjwa kwa makusudi na kulipiga picha ya X-ray na kisha kuikabidhi kwa kampuni ya bima kama sehemu ya dai na kwasababu bima hailipii gharama zote basi Wagonjwa walitakiwa kulipia salio lililopelea ambapo hiyo ikamfanya Daktari huyu ajipatie $318,600 (zaidi ya Tsh. milioni 700) kati ya $745,570 (zaidi ya Tsh. Bilioni 1.7) ambazo ni za madai ya kuanzia Januari 1, 2016 hadi Juni 28, 2018 ambapo tayari pia alipokea $114,294 (Tsh. milioni 264) ikiwa ni madai ya miezi sita ya kwanza kwa mwaka 2019.
Charmoli ambaye hukumu yake itasomwa June 17 2022 pia anakabiliwa na kesi za utovu wa afya katika Kaunti ya Washington Marekani kutoka kwa Wagonjwa karibu 100 na hii inaweza kumfanya afungwe zaidi ya miaka 20 jela.