Agizo la Rais Magufuli, kutaka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ‘TPDC’ kukamilisha makubaliano na kampuni ya Dangote Industries juu ya bei ya mauziano ya gesi asilia kwa ajili ya matumizi ya kiwanda hicho cha kutengeneza saruji kilichopo Mtwara limetekelezwa.
Leo April 20, 2017, Kaimu Mkurugenzi TPDC, Kapuulya Musomba ameeleza hatua iliyofikiwa mpaka sasa baada makubaliano juu ya kuunganishwa miundombinu ya kusafirisha gesi asilia kutoka kwenye bomba kubwa kwenda kwenye kiwanda cha Dangote pamoja na kinachoendelea kwa sasa.
“Mheshimiwa Rais alitoa maelekezo kusema kwamba mkubaliane na Dangote kwa ajili ya kuuziana gesi. Na katika muda aliokuwa ametoa, tuliweza kukubaliana kwa ajili ya namna ya kuuziana gesi na Dangote.” – Kapuulya Musomba.
Ufafanuzi zaidi juu ya makubaliano hayo, bonyeza play kwenye hii video hapa chini kutazama…
VIDEO: Mipango ya TPDC kusambaza gesi asilia DSM na Pwani. Bonyeza play kutazama.