Baada ya serikali kupiga marufuku unywaji na ufanyaji biashara ya vinjwaji aina ya viroba huku ikiweka sheria kwa wale watakaokiuka agizo hilo, Mbunge wa Sumbawanga mjini Aeshi Hilaly ameitaka serikali kuwalipa wafanyabiashara ambao tayari walikuwa wameagiza bidhaa hizo toka viwandani kabla ya agizo la serikali kutolewa.
Aeshi amesema>>>>>’Marufuku viroba ilikua haraka sana, kwa waliozuiliwa hatuna haki ya kuwalipa fidia?,Najua uchungu wa kufilisika, viroba tuzuie vinakotengenezwa ila Wafanyabiashara wavimalizie kwa kuuza mtaani‘
‘Kwangu Sumbawanga nina Wafanyabiashara watano wamekamatiwa viroba vyao, wamefilisika na nyumba zao zinauzwa,Sioni mantiki yoyote ya kitu halali mtu kanunua kiwandani alafu tunakataza ghafla viroba, watu wanaumia‘ –Aeshi Hilaly
Full video tayari nimekuwekea hapa chini mtu wangu….
VIDEO: Wizara ya muungano kutengewa zaidi ya Bilion 19 kama bajeti yake 2017/2018
BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo