August 27 2016 Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Simon Sirro amekutana na waandishi wa habari na kuongelea kwa ufupi taarifa za tukio la mashambulizi lililotokea Vikindu mkoa wa Pwani ambapo amesema taarifa kamili zitatolewa siku ya jumanne ikiwa ni pamoja na zile zinazodaiwa kuwa miongoni mwa wahalifu hao ni askari wastaafu.
'Dar ipo shwari na september 1 hali itaendelea kuwa shwari, nawasihi vijana wasiingie barabarani kuleta fujo' #Simon_Sirro
— millardayo (@millardayo) August 27, 2016
'Tuna taarifa za kiuchunguzi kwanba kuna watu wanapewa fedha kwa ajili ya kufanya fujo, nawasihi sana wasifanye hivyo' #Simon_Sirro
— millardayo (@millardayo) August 27, 2016
'Ukivunja sheria kwa kusudi sheria itachukua mkondo wake, tumejipanga vilivyo na tutashughulika nao' #Simon_Sirro
— millardayo (@millardayo) August 27, 2016
'Nasisitiza kwamba tuwaache wale wenye malengo yao waingie barabarani, tutawashughulikia ipasavyo' #Simon_Sirro
— millardayo (@millardayo) August 27, 2016
'Siku ya jana kulikuwa na operation kule Vikindu, kuna watu wameuawa na wengine wamejeruhiwa' #Simon_Sirro
— millardayo (@millardayo) August 27, 2016
Taarifa kamili kuhusu kilichotokea jana tutazitoa siku ya jumanne hivyo tunaomba uvumilivu wenu katika hili' #Simon_Sirro
— millardayo (@millardayo) August 27, 2016
'Ni lazima tusafishe Dar nzima iendelee kuwa salama siku zote na kazi bado inaendelea' #Simon_Sirro
— millardayo (@millardayo) August 27, 2016
'Siwezi kuongelea kama wahusika wa tukio la ujambazi ni miongoni mwa askari ama sivyo muda ukifika nitayaeleza yote' #Simon_Sirro
— millardayo (@millardayo) August 27, 2016
'Muda huu nimewapeleka askari wangu zaidi ya 80 ktk operation kuanzia Vikindu kuelekea Pwani na maeneo mengine ya Dar' #Simon_Sirro
— millardayo (@millardayo) August 27, 2016
ALICHOKIONGEA WAZIRI NCHEMBA BAADA YA KUFIKA ENEO WALIPOUAWA ASKARI DAR