Waziri wa ujenzi na Uchukuzi Prof Makame Mbarawa siku ya leo amekagua mradi wa ujenzi wa daraja la Tanzanite maarufu kama New Salendar bridge Akizungumza baada ya ukaguzi huo.
Waziri Mbarawa amethibitisha kukamilika kwa daraja hilo kwa asilimia 100 ambapo limegharimu zaidi ya Tsh bilioni 240 mbali na hayo waziri Mbarawa ametangaza kuanza kutumika kwa daraja hilo kuanzia siku ya jumanne Feb 1 mwaka huu na daraja hilo litatumika Bure kwa wananchi wote.