Wakazi wa vijiji vya Kisegese, Chiwachiwa na Lavina katika Kata ya Namwawala na Mbingu na Igima wataepuka hatari ya kupotezamaisha baada ya daraja jipya kuanza kujengwa katika Mto Luipa
Daraja linalotumika sasa ni la mbao linalodaiwa kukatika mara kwa mara na kusababisha vifo na majeruhi kwa
watumiaji wake.
Miongoni mwa miradi iliyipitiwa na mwenge na kuweka jiwe la msingi tayari kuanza maandalizi ya ujenzi wa daraja hilo linalogharimu Sh1.926 bilioni inayojumuhisha na barabara
Akizungunza katika uzinduzi huo uliofanyika katika Kijiji Cha kisegese ,, Mbunge wa Jimbo Mlimba, Mhe. Godwin Kunambi amesema wananchi wa vijiji hivyo wanapata madhara mbalimbali ikiwemo kutumbukia mtoni na kupoteza maisha, kujeruhiwa na wengine hupoteza mifugo na mazao mtoni hapo.
Mbunge huyo amesema kukamilika kwa
ujenzi wake kutaleta faraja zaidi kwa wananchi kwa kuwa linaunganisha pia vijiji vya Mbingu Chini, Kisegese, Chiwachiwa na Lavina.
Mkazi wa Kiii cha Kisegese, Scola Andrea (32) amesema mto Luipa una tabia ya kujaa kipindi cha masika na hakuna mtu anayeweza kuuvuka.
“Wanaopata shida zaidi wale wanaokaa Chiwawachiwa, maji yakijaa hapa huwezi
kuvuka na kama ndiyo mama mwenye mimba anataka kwenda kule ng’ambo hawezi kujifungua, atazalia hapahapa
mtoni,”
Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura), Mhandisi Sadiki Karume amesema ujenzi wa daraja la Luipa ulianza Mei 26, mwaka 2023 na unatarajiwa kukamilika Mei 28 mwaka 2024.
Amesema mpaka sasa ujenzi wake umegharimu Sh1.336 bilioni kati ya
Sh1.926 bilioni zitakazotumika kuukamilisha ujenzi wa daraja maboksi kabati matatu na kunyanyua tuta la barabara.
Mhandisi Karume amesema mkandarasi
anayetekeleza mradi huo ni kampuni ya Nabawy Construction Ltd ya Morogoro.
“Kukamilikia kwa daraja hili kutaleta nafuu kwa wananchi wa Kata ya
Namwawala na Mbungu,” amesema mhandisi Karume.
Akizungumza katika uzinduzi huo, kiongozi wa Mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa 2024 Godfrey Mnzava ameipongeza TARURA ngazi ya taifa na mkoa kwa kufuata taratibu za manunuzii na kumpata
mkandarasi aliyekidhi vigezo na kuondoa manung’uniko.