Katika pitapita zangu leo nikakutana na hawa jamaa wanaotengeneza Traffic lights maeneo ya Morogoro road, kiukweli panapendeza sana.
Siku chache zilizopita kiongozi wa kampuni ya Strabag aliongea kupitia TBC1, akaeleza kuwa taa watakazotengeneza ni za kisasa zaidi ambazo watazifunga kwenye Barabara za mwendokasi na zitakuwa na Sensor.. yaani itakuwa hivi; kama basi la mwendokasi linakaribia, taa zitazuia gari nyingine automatic na basi la mwendokasi litapita bila kusubiri foleni.
Cheki hizi pichaz zinazoonesha shughuli ya kufunga taa ikiendelea Dar es Salaam July 08 2015.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.