Mabingwa wa Premier League walikuwa wametoa ofa ya £80m mbele pamoja na £10m za nyongeza huku Arsenal ikiwa bado wanashinikiza kumsajili Rice na West Ham wanatarajia kuja na ofa ya tatu baada ya ofa mbili kukataliwa.
Arsenal walikuwa na ofa ya £90m ambayo ni rekodi ya klabu inayojumuisha ada ya £75m na nyongeza ya £15m – iliyokataliwa na wapinzani wao wa London mapema mwezi huu baada ya ofa yao ya ufunguzi iliyodhaniwa kuwa ya thamani ya £80m pamoja na nyongeza pia kukataliwa.
Thamani ya West Ham kwa Rice inasalia kuwa £120m lakini inaeleweka klabu hiyo itakubali £100m pamoja na mchezaji.
Rice ataondoka West Ham mwishoni mwa msimu baada ya kiungo huyo kuwa nahodha wa klabu hiyo kutwaa taji lao la kwanza la Uropa katika kipindi cha miaka 58.
Makubaliano ya kiungwana yanamaanisha Rice anaweza kuondoka licha ya mwaka mmoja uliosalia kwenye kandarasi yake na chaguo la kuongeza kwa miezi 12 zaidi.