Nyota kutokea nchini Davido ametangaza kutoa msaada wa Naira milioni 300 ambazo ni sawa na kiasi cha shilingi milioni 470.1 za kitanzania kusaidia waathirika wa dawa za kulevya pamoja na watoto yatima nchini kwake wakati akisherehekea siku yake ya kuzaliwa
“kwa mara nyingine tena siku yangu ya kuzaliwa mwaka huu tunakwenda kuchangia kwa watoto yatima pamoja na taasisi ya kusaidia vijana wenye umri mdogo kuacha matumizi ya dawa za kulevya na mwaka huu ni naira milioni 300” Anaandika davido katika ukurasa wake wa X
Ni utaratibu wa davido kufanya hivyo kila ifikapo nov 21 siku yake ya kuzaliwa na mwaka huu anatarajia kufanya show yake ya kusheherehea siku yake ya kuzaliwa #atlanta nchini marekani.
Davido alianzisha ya Davido Adeleke Foundation mnamo 2022 kwa msaada wa mashirika mengine ya hisani, kwa nia ya kusaidia watoto walio katika mazingira magumu.
Mnamo Julai 2023, alitangaza taasisi hiyo ilitoa zaidi ya N200 milioni kwa vituo vya watoto yatima nchini na watoto 13,818 walinufaika nayo.
Pia aliahidi kutoa pesa zaidi mnamo 2024.