Baraza la tiba Asili Zanzibar kwa kushirikiana na wakala wa Chakula na Dawa ZFDA limekamata Dawa za Binadamu za Hospital ambazo zimekutwa kwenye duka la dawa za Asili huko kwa Haji Tumbo Mkoa wa Mjini dawa ambazo hazihitajiki kuuzwa kwenye maduka ya asili na hutakiwa kuuzwa na kutolewa na mtaalumu wa afya
Dawa hizo mchanganyiko zikiwemo dawa za nguvu za kiume zinazouzwa holela zinazoweza kuuzwa hata kwa vijana wadogo ambazo matumizi yake hutakiwa kutumiwa na watu wazima ambao umri umeenda pamoja na wenye sukari ,presha na dawa zenye kemikali kubwa na dawa nyingine zilizoishiwa muda wa matumizi
Mrajisi Baraza la tiba asili Zanzibar Mohammed Mshanga amewasaa watumiaji wa dawa hizo kuacha kununua dawa kiholela pasii na kuandikiwa na wataalumu wa afya na kufikia uwaamuzi wa kulifunga duka hilo kwa kukiuka utaratibu zilizoekwa kwenye maduka ya kuuza dawa za asili
Kwa upande wake mfanyabiashara wa Duka hilo Bi Mwatima ameomba radhi kwa kukiuka utaratibu huo uliokweka na kuiyahidi mamlaka hiyo kufuata tararibu zilizoekwa na serikali kupitia Baraza la tiba Asili na wakala wa dawa na Chakula ZFDA