Mamlaka ya mji wa Hejiang chini China umekuja na utaratibu mpya na wakiubunifu wa kukabiliana na wale wote ambao wanakataa kulipa madeni yao ambapo majina na sura ya wadaiwa huoneshwa kwenye majumba ya sinema kabla ya filamu yenyewe kuanza.
Ili kuleta ufanisi wa zoezi hilo ambao unajulikana kama “Real of Shame” mamlaka hiyo huonesha vipande hivyo vya video vyenye taarifa za wadaiwa katika majumba ya sinema ya maeneo wanapoishi wadaiwa hao ili kuhakikisha ujumbe unawafikia walengwa.