Benki ya Exim imeibuka kinara wa kutunza na kuhifadhi mazingira miongoni mwa taasisi za kifedha jijini Dar es Salaam na hivyo kukabidhiwa tuzo maalum ya kutambua jitihada hizo kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Tuzo hiyo maalum imekabidhiwa hii leo na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amosi Makala katika sherehe za kuadhimisha siku ya Mazingira duniani zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Kupitia mkakati wake wa kutunza na kuhifadhi mazingira unaofahamika kama ‘Exim Go Green Initiative’ benki hiyo imekuwa mstari mbele katika kampeni mbalimbali za kuhifadhi mazingira ikiwemo upandaji miti ambapo hivi karibuni benki hiyo kwa kushirikiana na Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda ilipanda miti 10,0000 jijini Dodoma
Aidha, benki hiyo pia imekuwa imekuwa mstari wa mbele katika utunzaji wa bustani mbalimbali zilizopo kwenye baadhi ya majiji hapa nchini ikiwemo Dar es salaam.