Mawakili zaidi ya 20 wamekutana katika Tamasha la kutatua matatizo ya kisheria na elimu kwa wananchi baada ya kuwepo kwa kesi za mirathi, migogo ya ndoa na Ardhi katika Wilaya ya Njombe
Mkuu wa Wilaya hiyo Kissa Kasongwa akishrikiana na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii NSSF, Bohari ya Dawa MSD ameamua kufanya Tamasha hilo baada ya ziara ya kutembelea mahabusu na jamii ya wananchi wa Njombe ambapo alibaini kesi za aina hiyo zinazogharimu maisha ya wananchi wa wilaya hiyo.
Tamasha limebeba kauli mbiu ya Njombe ya Mama Samia lililoburudishwa Mrisho Mpoto, Khadija Kopa na Msaga Sumu limeambatana na utoaji wa mkopo wa Bilioni 1,204,500,000/= ulikabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Marwa Rubirya kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na wenye ulemavu.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Njombe Marwa Rubirya akisistiza chanjo ya Corona amesisitiza Wakurugenzi kusimamia miradi inayojengwa kwa fedha za Uviko 19 inayotakuwa kukamilika mwezi desemba 2021.