Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Halima Bulembo ameiagiza Idara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Idara ya Mapato Manispaa ya Kigamboni kuanza kufatilia kwa Kina mapato yanayotokana na Kisiwa cha Sinda kwani ni njia mojawapo ya kuongezea pato la Manispaa.
Mkuu wa Wilaya DC Bulembo ameyasema hayo leo wakati wa ziara ya kuwatembelea wavuvi katika kata ya Somangila na Mjimwema kwa kusikiliza na kupokea changamoto zao huku lengo kuondoa changamoto katika sekta hiyo nchini.
” Huu ni Wakati wa Maafisa wote wa Idara husika kuangalia kwa kina namna mapato ya Manispaa yetu tunayaongeza kupitia Kisiwa cha Sinda pamoja na Shughuli nzima za Uvuvi katika Manispaa, Wakuu wote wote mtoke ofisini muanze kufatilia Kama Ilivyo kwa Visiwa vingine kama Mbudia kule Kinondoni ” Amesema Halima Bulembo.
Aidha Bulembo kaendelea kutoa msisitizo kwa kumepiga marufuku tabia zinazofanywa na baadhi ya Wazazi ama Walezi ambao wanawatumia watoto kama njia mojawapo ya kujipatia kipato kwa biashara ndogo ndogo haswa nyakati za mchana ambapo wanapaswa kuwa shuleni kwani ni makosa kisheria.
” Miongoni mwa vitu vya msingi vya mtoto ni kwenda shule sasa inakuwaje mzazi unamruhusu mtoto afanye biashara wakati wa Shule, Sisi kama Serikali hatuogopi kumchukulia hatua Mzazi ama Mlezi akiwa anamtumikisha matoto ” Amesema Bulembo.