Katika kukuza na kuboresha sekta ya Ufugaji na Uvuvi nchini, Halmashauri ya Wilaya ya Kigamboni chini ya Mkuu wa wilaya Halima Bulembo wamefanya ziara ya kuwatembelea Wavuvi katika Maeneo ya Pembamnazi na Kimbiji kwa lengo la kubaini changamoto zao na Kuzitatua.
Wakati wa Mawasilisho yao, Wavuvi wa Pembamnazi na Kimbiji wameiomba Serikali ya Wilaya ya Kigamboni kuanza Kuwapatia Leseni zenye ubora sambamba na Elimu nzuri juu ya Namna ya kuvua Samaki ili kuepukana na Uvuvi haramu.
Hata hivyo naye Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Halima Bulembo amewatoa hofu Wavuvi hao juu ya Namna ya Kupata Leseni zenye Ubora lakini pia ametoa maagizo kwa Maafisa Uvuvi na Ufugaji kuanza kupita katika maeneo ya Beach na kuanza kutoa Elimu kwa lengo la kuepukana na Uvuvi haramu.
Sambamba na hayo mkuu wa wilaya ya Kigamboni, amewasihi Wavuvi kuendelea kuzingatia Usafi katika maeneo yao ya kazi kwani inafaida ya kuwavutia zaidi wateja kama maeneo yatakuwa safi yatavutia pia Wanunuzi.