Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mhandidi Maryprisca Mahundi ametatua mgogoro wa mpaka baina ya Vijiji vitatu vinavyogombania Kitongoji cha Wafugaji kiitwacho Simba leaf na kuhatarisha amani ya eneo hilo.
Vijiji vilivyokuwa kwenye mgogoro huo ni Mbugani, Chalangwa na Sangambi ambavyo kila kimoja kilikuwa kikidai Kitongoji cha Simba Leaf kinachokaliwa na watu jamii ya wafugaji na ni mali yao.
Hali hiyo ikasababisha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo ikiongozana na Maofisa Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya kwenda kutatuta mgogoro huo kwa kutumia ramani iliyoboreshwa kwa mara ya mwisho mwaka 2006 wakiitafsiri kwa kutumia kipimo cha GPS.