Ni Octoba 5, 2023 ambapo Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Jabiri Makame yuko kwenye kipindi cha Power Breakfast ya Clouds FM muda huu.
Hizi ni nukuu zake kuhusu tusiyoyajuak kuhusu Gairo.
“Gairo ni Wilaya ambayo tupo karibu sana na Dodoma na Dodoma ndio makao makuu ya nchi, mtu akitaka kwenda kufanya utalii na kupumzika Gairo ni sehemu sahihi sana’-
“Tumejipanga kwa sasa hivi tunaboresha mazingira ili watu watakaokuja kutembelea Maeneo yetu ya utalii wapate kile ambacho wanakitarajia kukiona kulingana na uasili wake” Mkuu wa Wilaya ya Gairo Jabiri Makame
“Ni kweli Vinyonga wenye pembe wanapatikana Gairo. Wapo Vinyonga wenye pembe Mbili, Tatu hao wote wanapatikana kwenye msitu wetu wa Ukagulu ambao ni msitu wa hifadhi wa mazingira yetu ya asili. Lakini pia sio tu Vinyonga mliowazungumzia pia kuna water falls (maporomoko ya maji). Pia kuna ndege ambao hawapatikani katika Maeneo yoyote ya duniani. Pia wapo wale panzi wenye rangi za bendera ya Taifa” Mkuu wa Wilaya ya Gairo Jabiri Makame
‘Changamoto kubwa ambayo sisi kama viongozi tumeiona kwanza inaanzia kwenye tija productivity ni kwamba wananchi wengi wanazalisha lakini ukija kwa mwananchi mmoja mmoja anazalisha kwa kiwango gani? Wataalamu wa kilimo wanasema kwenye eneo la ekari moja ambapo mtu analima mahindi akifuata kanuni bora za kilimo anapaswa kuzalisha gunia kati ya 20 hadi 25. Kwa hali ilivyo sasa hivi wananchi wanazalisha chini ya gunia tano kutokana na kutokufuata kanuni bora za kilimo lakini pia changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi’- Mkuu wa Wilaya ya Gairo Jabiri Makame
“Na wengi wanauza mahindi badala ya kuongeza thamani kwa kuuza unga ambao una soko zuri zaidi kuliko kuuza mahindi ambayo yanakuwa bado hayajaongezewa thamani” Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Jabir Makame
View this post on Instagram