Kutoka Temeke hii ni video ya Drone ya muonekano wa eneo la mbele ya Uwanja wa Mkapa baada ya kuwekwa kwa taa za kisasa 32 ili kukomesha wizi uliokuwa unasababishwa na giza nene katika eneo hilo, zoezi la ukarabati na uwekaji taa hizo limegharimu zaidi ya Tsh. Milioni 102.
Itakumbukwa wiki mbili zilizopita Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo alitoa taarifa kuwa amedhamiria kubadilisha taswira ya muonekano wa eneo la mbele ya Ofisi DC ambalo linatazamana na Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa kuweka taa za kisasa 32 ambapo tayari zoezi la kuweka taa hizo limekamilika kwa 100%.
DC Jokate alisema eneo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya linatazamana na Uwanja wa Benjamin Mkapa ambalo hukutanisha Maelfu ya Watanzania na Watu wa Mataifa mbalimbali, hivyo ni vizuri taswira yake ikaendana na hadhi hiyo.
Alisema ana taarifa za uhalifu nyakati za usiku ambapo eneo hilo kwa kukosa taa huwa na kiza kinene, kinachopelekea wepesi wa vitendo viovu kufanyika—“Mimi ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Temeke haitaleta afya hata kidogo uhalifu kufanyika eneo la Ofisi ya DC ”
UNAWEZA UKATAZAMA MAAGIZO YA DC JOKATE KABLA YA KUBORESHWA KWA ENEO HILO AMBALO KWASASA LIMEWEKWA TAA ZA KISASA