Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo ameoneshwa kutopendezwa na video inayosambaa mtandaoni ikimuonesha Mfanyabiashara Aristote ambaye pia ni Rafiki wa Mwigizaji Irene Uwoya akizungumza kuhusu Mwigizaji Wema Sepetu kupanda Taxi kutokana na kutokuwa na gari huku Irene Uwoya akimiliki Range Rover.
Baada ya kuitazama video hiyo Jokate aliandika ——> “Ifike muda sheria ifuate mkondo wake kukomesha tabia na hulka za aina hii kwenye jamii zetu, iwe funzo kwa wote na msamaha pekee yake hautoshi, Watu wanajiua kwa kuwa bullied online, this has to stop!!!”
Kwenye video hiyo Mfanyabiashara Aristote alisikika akisema “kipato huwa hakijifichi, kwa mfano tu Irene anaendesha Range Wema anatumia Uber, Bolt, hana usafiri… mwenzie Irene anatumia Raaaaaange” ambapo baada ya kusambaa kwa video hii Mfanyabiashara huyo aliomba msamaha kwa kuandika “samahani sana my Sister🙏”
Wema Sepetu aliipost video hiyo saa kadhaa zilizopita na kuandika ——> “Wacha nikuweke kabisa kwa page yangu upate kufurahi maana nimekaa sana mdomoni mwako, kurequest nako ni K vilevile maana nakutanaga na Mashabiki pia, miaka miwili sasa sina gari na mbona maisha fresh tu, mkitembelea nyinyi ma Range inatosha Aristotee… sio mbaya….🙏🏼🙏🏼🙏🏼 Ila ifike muda mnipumzishe basi maana Im nat in a competition na Mtu yoyote in my life, sijawahi kushindana na Mtu”
Naye Mwigizaji Irene Uwoya alitumia ukurasa wake kumpa pole Wema na kukanusha kumtuma Mfanyabiashara huyo ——>“Binafsi Nimesikitishwa sana na maneno yasiyo ya kibinaadamu yaliyotolewa na Aristote dhidi ya Wema’- Irene Uwoya
“Watu waelewe kitu kimoja leo, sijawahi kumtuma Aristote amtukane Wema wala Mtu yeyote yule, sina ugomvi na Wema na sina sababu ya kufanya upuuzi wa namna hiyo, nimempigia pia Aristote kuoneshwa kukasirishwa kwangu na niseme tu hiyo ni MIHEMKO yake yeye, sihusiki na lolote juu ya hayo aliyoyaropoka ambayo yanaleta hata uchonganishi baina yetu kitu ambacho sikifurahii kwakweli, kingine nichukue nafasi hii kukupa Pole Wema kwa haya yaliyotokea, hata mimi ningekuwa wewe ningejiskia kama unavyojiskia, pole sana sana”- Uwoya