Kitakachowagusa wananchi wa chini ni huduma bora tutakazotoa, tutoe huduma sawa kwa wananchi bila kuwa na matabaka kwa kufanya hivyo miundombinu iliyoboreshwa katika Hospitali hii ya Mji Mafinga iliyojengwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu itafanya wananchi kupata huduma bora na kuisemea Serikali vizuri”
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Dkt. Linda Salekwa alipokuwa akizindua zoezi la Upandaji wa Miti katika Halmashauri ya Mji Mafinga ( MTI WA MAMA) zoezi lililofanyika Katika Hospitali ya Mji Mafinga kwa kushirikisha wadau wa PRESHDAS Company Limited ambao wametoa jumla ya miche 570.
Amesema Majengo yaliyojengwa katika Hospitali ya Mji Mafinga yataenda kuwa na maana kama mazingira ya Hospitali na huduma yatafanana na majengo.
“ Tuhakikishe mazingira yanayoizunguka Hospitali ya Mji Mafinga yanaendelea kuboreshwa kwa kupanda ukoka, maua na kuweka maeneo ya kupumzika kwa wagonjwa
Aidha Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya Amempongeza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mheshimiwa Regnant Kivingena Mkurugenzi Mji Bi . Fidelica Myovella kwa kuamua kuchagua Hospitali ya Mji Kupandwa Miti na kupongeza kwa kujenga jengo la Kuifadhia Maiti na jengo la wodi ya daraja la kwanza( VIP) kwa kutumia fedha za mapato ya ndani.
Naye Afisa Mafunzo na Usimamizi wa Rasilimali watu kutoka PRESHDAS, Ndugu. Geofrey Nyakunga amesema Taasisi hiyo ni mdau wa Mazingira na inajishughulisha na uhifadhi wa mazingira, kusimamia mashamba, kufanya tathmini ya mashamba kabla ya uvunaji na kutoa elimu kwa wakulima.
Amesema katika zoezi hili la uzinduzi wa Upandaji Miti kwa Halmashauri ya Mji Mafinga PRESHDAS wametoa miche 570 , miche 70 ya matunda na miche 500 ya kivuli na mpaka leo tarehe 27 Januari, 2025 jumla ya miche 762,376 ya matunda, mbao imepandwa maeneo mbalimbali katika Halmashauri na zoezi linaendelea.