Mkuu wa Wilaya ya Gairo ndugu Jabiri Makame, July 6, 2024 ametunukiwa TUZO YA HESHIMA na Wizara ya Kilimo, Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania, kwa Kuwa “MDAU WA USHIRIKA MWENYE USHAWISHI NA UHAMASISHAJI MKUBWA KATIKA MASUALA YA USHIRIKA KWENYE JAMII”.
Tuzo hiyo imetolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dotto Biteko, katika Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika kitaifa Mkoani Tabora.
Wilaya ya Gairo ni Moja ya Wilaya ambazo zimekuwa zikifanya kazi kubwa ya kusimamia Uanzishaji wa Vyama vya Ushirika ikiwa ni nyenzo muhimu ya Maendeleo ya Kilimo katika Wilaya hiyo. Zaidi ya asilimia 98% ya Wananchi wa Gairo wamejiajiri katika Sekta ya Kilimo na Mifugo, hivyo Sekta hizi ndiyo mhimili wa Uchumi wa Wilaya na Msingi wa Kupambana na Umasikini na Kuongeza Ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri.
Kwa kuzingatia hayo, Wilaya inafanya kazi kubwa ya kuhamasisha wakulima kufanya Kilimo Bora ili kuongeza Tija na Uzalishaji.
Ili kufanikisha adhma hiyo katika Wilaya ya Gairo Sekta ya Ushirika inatazamwa kama nyenzo muhimu katika Kukabiliana na Changamoto zinazokwamisha wakulima katika safari ya Mageuzi ya Sekta ya Kilimo. Changamoto hizo ni pamoja na upatikanaji wa mbegu bora, mbolea, Viuatulifu, Masoko, elimu duni ya kufanya Kilimo Bora, ukosefu wa mitaji, zana duni za Kilimo nk.
Changamoto hizi na zingine zinaweza kutatuliwa kwa haraka na urahisi kupitia Vyama vya Ushirika. Hivyo, Wilaya ya Gairo imefufua na inaendelea kuhamasisha Maendeleo ya Ushirika katika Sekta ya Kilimo ili kuwakomboa wakulima. Aidha, kazi ya kujenga Ushirika Gairo haiishii kwenye Kilimo pekee bali inagusa Sekta zingine ikiwemo Wafugaji, Wafanyabiashara, Makundi ya Wanawake, Vijana, Watumishi nk.
Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Ushirika Mwaka.