Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Judith NGuli amewahakikishia wakulima wa mpunga skimu ya umwagiliaji Dakawa (UWAWAKUDA) kuwa Serikali itahakikisha inatatua changamoto zinazowakabili ikiwemo soko la uhakika la zao hilo.
DC Ngulli amesema kutokana na umuhimu wa skimu hiyo katika uzalishani chakula nchini Serikali ipo mbioni kuwatafutia soko hata nje ya nchi ili waweze kunufaika kupitia Sekta hiyo.
Amesema skimu hiyo licha ya kuwapatia kipato Wakulima hao lakini Wilaya pia inategemea kuanza Kulima kwa ajili ya kuwapatia Chakula shuleni Wanafunzi hivyo ni lazima uboreshaji wa Miundombinu pamoja na masuala mengine yafanyike ili kuwainua kiuchumi.
Changamoto Zingine wanazowakabili Wakulima hao ni suala la ongezeko la ndege waharibifu aina ya kwerea kwerea ambao wanashambulia mpunga jambo ambalo Serikali imeahidi kupiga sumu ili kuwateketeza angalau mara mbili kila mwaka.
Kwa Upande wake mwenyekiti wa skimu hiyo Charles Pangapanga anasema endapo Serikali itawapatia soko la uhakika watapiga hatua kiuchumi kutokana na kuzalisha mpunga kwa wingi katika mashamba hayo.
Amesema mpango wa Umoja huo ni kuanzisha Kiwanda cha Mpunga ili kuanza kuuza mchele ,na pumba kutengeneze. Chakula cha mifugo pamoja na utengenezaji wa mkaa kuokoa uharibifu wa mazingira.