Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Abdallah Mwaipaya amekamata ngamia 89 wakisafirishwa bila utaratibu na Watu wanne waliokua wakiwaswaga ngamia hao kuwa na utata kuhusu uraia wao.
“Baada ya kupata taarifa hii tumegundua kuna vibali vipo ila kuna utata, tumebaini hawana vibali vinavyowawezesha kuwa hapa nchini, tutawaweka hapa ngamia hao na watakuwa chini ya Serikali ya kijiji, kuna watu wa uhamiaji wanaenda kuangalia document zao kujua uhalali wao” DC Mwaipaya.
“Same wanakopelekwa ni mbali, hatuwezi kuwaruhusu wapelekwe kwa miguu au wawapitishe barabarani kwa sababu kote huko wanaweza kusababisha matatizo mengine ikiwemo kula kwenye mashamba ya Watu” DC Mwaipaya