Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya amefika Kanisani katika Kijiji alichozaliwa cha Sambasha Wilayani Arumeru na kuwashukuru wananchi kwa kumuamini na kumchagua mwaka 2015 kuwa Diwani bila kujali udogo wake na desturi za jamii ya Kimaasai.
Sabaya katika ibada hiyo amemshukuru MUNGU kwa kuaminiwa na Rais Magufuli katikati ya nyakati ngumu huku akisema “Kuteuliwa na Rais ni jambo moja lakini kuteuliwa na Rais aina ya Magufuli na kuaminiwa ni jambo lingine”.
Aidha Ole Sabaya ametangaza kutongembea nafasi yoyote ya Ubunge wala Udiwani hata kama anazisikia sauti zikimuelekeza huko na kusema imani aliyopewa na Rais ataendelea kuitendea haki na kwamba kutafuta nafasi zingine kwake ina tafsiri ya kutoridhika kwani kama ni kutumika anaweza watumikia hata wao katika nafasi hiyo.