Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe.Hashimu Mgandilwa ameitaka jamii kuenzi tamaduni zilizopo hapa nchini ili kuweza kuwa na taifa lenye kutunza mila na desturi zetu.
Akizungumza na wanahabari leo Mkuu wa Wilaya Mgandilwa amesema kuwa lengo la Tamasha la Tanga Utalii Festival ni kuonesha jamii umuhimu wa kuenzi na kutunza tamaduni zilizopo hapa nchini hususani Mkoa wa Tanga na kutangaza vivutio vilivyopo Mkoani Tanga.
“Tanga tuna maeneo megn iya utalii kwa mfano tuna mapango ya Amboni wengi tumesoma kwenye historia lakini bado hatujapata fursa ya kwenda kutembelea hayo mapango pamoja na hiyo tuna mambo ya kitamaduni na vitu vingi sana”- DC Hashimu Mgandilwa
“Pamoja na hilo Serikali inafanya uwekezaji mkubwa sana katika maeneo yetu haya ikiwemo ujenzi wa wa barabarani ya Pangani ambapo kule kuna fursa mbalimbali ya maeneo ya utalii”– DC Mgandilwa
“Hayo ni maeneo machache kwahiyo tuliona hakuna aliyeweza kutangaza hayo maeneo sasa kupitia Ofisi yangu iliona ni vymea kuandaa tamasha maalum la Utalii ili kupanua fursa za kiuchumi zilizopo katika Mkoani wetu“- DC Mgandilwa
“Kupitia Tamasha hili kutampa mwananchi kujifunza fursa mbalimbali kupitia tamaduni zet, kwahiyo Tanga kumenoga nawakaribisha Machi 26, 2022 mahali ni Tanga Urithi mbali na fursa lakini pia kutakuwa na burudani atakuwepo Dula Makabila, Kassim Mganga, – DC Mngandilwa
NOMA!! TAZAMA MAZOEZI YA TWAHA KIDUKU SIO YA KITOTO, ANENA PAMBANO LAKE NA MCONGO