Serikali ya Tanzania imesema inatarajia kumaliza tatizo la kukatika kwa umeme pamoja na kupunguza gharama za upatikanaji wa nishati hii, ni ahadi ambayo imetolewa na Waziri wa Nishati Prof. Sospeter Muhongo alipofanya ziara kwenye kituo cha kuzalishia umeme cha Mtera mpakani mwa Dodoma na Iringa.
Baada ya kuona kina cha maji kimepungua Mtera na uzalishaji umesimama waziri Muhongo amesema ‘Tunataka Mtera ifanye kazi, suluhisho ni lipi? itabidi tukae chini kukubaliana management ya haya maji, pia kuongeza vyanzo vingi vya umeme ambavyo tayari tumeshaongeza ili tuache haya mabwawa angalau kwa mwaka mmoja au miwili yaweze kujaa kufikia kina ambacho kilikuwepo mwaka 1988′
KAVUMBAGU KAUZWA NA AZAM FC?
Jibu lililotolewa na msemaji wa Azam Jaffary Idd ni hili >>> ‘Watu wengi wanaisemea Azam nje, Kavumbagu ana mkataba na Azam na tulishasema yeyote anaemtaka aje tufanye biashara na atamchukua, sisi hatuzuii mchezaji yeyote kwenda kwengine‘
Bonyeza play hapa kwenye hii video uzipate hizi stori kwa urefu wake..
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.