Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa ameitisha Wananchi wote wa Wilaya hiyo kuja kusikilizwa kero zao kwa pamoja na kutatulia baada ya kuita Taasisi zote ambazo zipo ndani ya Wilaya hiyo na nje huku akiwa kaita Mawakili zaidi ya 40 ambao kazi yao itakua ni kutoa ushauri wa kisheria kuhusu migogoro ya Ardhi, ndoa na mirathi na mambo mengine.
Wabunge wa Korogwe Mjini na Vijijini wamesema wao kama Wawakilishi wa Wananchi wakienda kuwasikiliza wananchi wao wananapata kero nyingi ikiwemo migogoro ya ardhi na uhaba wa vitambulisho vya NIDA na vya kuzaliwa na imekuwa changamoto kwa wananchi hivyo tukio hilo ni la kwanza kutokea katika Wilaya hiyo na kuweka historia.
DC KOROGWE AWAVAA VIONGOZI HADHARANI, ATANGAZA KUWATUMBUA “NAKAA PARKING SIKAI OFISINI”