Kuna malalamiko mengi tumekutana nayo kuhusu ishu ya Mahakama au vyombo vingine vya Kisheria kushindwa kutoa utatuzi wa matatizo mbalimbali yanayowapata watu.
Kama ulidhani msaada wa Kisheria tatizo lake linaishia Mahakamani pekeyake, basi nakusogezea ujumbe kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ambaye kathibitisha kwamba hata hiyo ishu ikifika kwenye ngazi yake pia inaweza kupata ufumbuzi.
“Sheria ya mwaka 2011 imeongelea utaratibu wa Wilaya kushughulika na nidhamu ya mahakama… Changamoto kubwa katika taifa letu ni malalamiko ya wananchi juu ya huduma wanazozipata wanapokwenda kwenye mahakama, bahati mbaya hawajui kama kuna chombo kingine wanachoweza kukikimbilia na wakapata haki zao“- DC Paul Makonda.
“Tangazo langu ni kuwaambia watu wa Kinondoni wote wanayo haki ya kuja Wilayani na tutawasikiliza na hatua zitachukuliwa kwa wale watakaopatikana na hatia‘ >>> Paul Makonda.
Sauti ya Mkuu wa Wilaya, Paul Makonda hii hapana majibu yote kuhusu ishu ya matatizo Kisheria pia.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTERFB YOUTUBE.