Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Ulanga imewakamata watu wawili Erick Samwel na Exprius Kwilinga kwa tuhuma za kutengeneza Madini feki aina ya Vito na kuyauza kwa wafanyabishara .
Mwenyekiti kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Ulanga ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Ngollo Malenya amesema wafanyabishara hao wamekamatwa baada ya Wananchi kulalamika kutapeliwa kuuziwa Madini feki.
Dc Malenya amesema Wafanyabishara hao wamekuwa wakichukua mawe kisha kuyapaka wino wa peni na kukausha juani mawe hayo na baada muda kuyauza katika soko la Madini wilayani humo.
Watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa na upelelezi utakapokamilika watafikishwa katika mamlaka husika kujibu tuhuma zinazowakabili.
WAWILI WAKAMATWA WAKIUZA MADINI FEKI, “WANAYAPAKA WINO KUWADANGANYA WATU KUWA NI MADINI, MILIONI 3”
HARMONIZE AMPA ONYO KALI MWIJAKU, AMWAMBIA “HILI SUALA LIACHE TU, HAKUNA ALIYEKAMILIKA”