Leo December 28, 2017 Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Dr. Charles Kimei amezungumza na waandishi wa habari na kuweka wazi nia yake ya kuachia kiti hicho ifikapo mwezi May mwaka 2019.
Ameeleza kuwa mchakato wa kutafuta Mkurugenzi mpya utaanza hivi karibuni na kwamba ataaga rasmi muda ukifika na taarifa rasmi itatolewa hivi karibuni lakini kwa sasa ameamua tu kutoa ufupi tu wa taarifa hiyo.
Dr. Kimei ameiongoza taasisi hiyo ya benki kwa takriban miaka 2o sasa na anapostaafu atakuwa ametumikia CRDB kwa miaka 21. Ameeleza kuwa kuachia kwake ngazi kutawapa nafasi watu wengine kutumia uwezo wao kuiogoza CRDB.
Paul Makonda akabidhiwa milioni 15 na CRDB