Iwapo mtumiaji atahama na kupewa laini mpya na zikapita siku 30, je itabidi afuate utaratibu uleule kurudi kwa mtoa huduma wa awali?
Ndiyo. Kila mara mtumiaji anapotaka kuhama na namba yake, atatakiwa kwenda kwenye ofisi za huduma kwa wateja, kwa wakala wa mtoa huduma au kwa mtoa huduma wa mtandao anaotaka kuhamia kuomba kuhamia mtandao huo.
Atahitajika kupewa laini mpya ya simu. Iwapo mtumiaji anarejea kwa mtoa huduma wake wa awali, atahitajika kupata laini mpya kutoka kwa mtoa huduma wa awali na hivyo kufanya laini yake ya zamani kutokufanya kazi?
Mtumiaji atahitajika kupewa laini mpya ya simu kila mara anapohama kwenda kwa mtoa huduma mpya kwani laini yake ya zamani haitaweza kutumika kwenye mtandao mpya.
Je mtoa huduma wa sasa wa mteja anaweza kujaribu kumshawishi abakie naye wakati akitaka kuhama? Hapana. Mtoa huduma wa sasa wa mteja hatakiwi kuwasiliana naye wakati wa mchakato wa kuhama ili kujaribu kumshawishi kubakia kwake.
Iwapo hilo litatokea mteja anatakiwa kutoa taarifa kwa mtoa huduma wake mpya.
Mteja atoe taarifa wapi iwapo mtoa huduma wa mteja atampigia simu au kumsumbua kama njia ya kumtaka arejee kwenye mtandao wake ndani ya siku 30 baada ya kuhama?
Mteja anatakiwa kutoa taarifa kwa mtoa huduma wake mpya. Ni namba zipi zinazoweza kuhamishwa? Namba yoyote ya simu za kiganjani inaweza kuhamishwa bila kujali inatumiwa kwa aina gani ya huduma – mfano maongezi, meseji, data, kujua maeneo kijiografia kwa mfumo wa GPS na kadhalika.