Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma imeamuru kurudishwa tena rumande hadi December 19, 2017 kwa aliekuwa Mwenyekiti wa UVCCM na Mbunge wa Donge, Zanzibar Sadifa Juma Khamis.
Mwenyekiti huyu alikamatwa nyumbani kwake Dodoma December 9, 2017 kwa tuhuma za Rushwa, kwamba alikamatwa akiwapa Wajumbe soda kutoka Kagera na kosa la pili aliwaahidi kuwalipia nauli.
Wakili wake Godfrey Wasonga amezungumza na Waandishi nje ya Mahakama na kusema “Sadifa anashtakiwa kwa kosa la Rushwa, kutoa hongo kwa baadhi ya Wajumbe, kwa leo kulikua na hoja.. ana makosa mawili lakini yote yanaruhusiwa dhamana”
“Makosa ambayo ni ya uhujumu uchumi ambayo yapo kwenye sheria ya Rushwa lakini sheria hiyo haizuii mtu kupewa dhamana, dhamana inaweza kuzuiliwa kwenye makosa ya mauaji”
Mtazame Sadifa mwenyewe alivyofikishwa Mahakamani na kila kitu alichosema Wakili wake, bonyeza play hapa chini
VIDEO: KITU JPM AMEONGEA KUHUSU MWENYEKITI WA UVCCM ALIEKAMATWA KWA TUHUMA ZA RUSHWA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA
“HAKUNA CHENYE MWANZO KISICHO NA MWISHO” – WEMA SEPETU AWEKA HII AKIWA NA MAKONDA